JUMAPILI ya leo Julai 10 ni miaka mitatu kamili imetimia tangu aliyekuwa mwandishi chipukizi wa Gazeti la Spoti Xtra na Championi Ibrahim Mressy afariki dunia.
Ilikuwa ni Julai 10,2019 taarifa za kutangulia kwake mbele za haki zilifika katika kituo chake cha kazi Gloal Pulishers,baada ya kuugua ghafla.
Mbali na kuandikikia Magazeti ya Championi na Spoti Xtra,Mressy pia alikuwa na kolamu yake ya Michezo na Burudani kwenye Gazeti la Ijumaa.
Familia ya michezo bado inakumbuka mchango mkubwa wa Mressy kwa namna ambavyo alikuwa anapenda kujituma na kufundisha wengine waliokuwa wakihitaji kujifunza.