UCHAGUZI YANGA LEO,RAIS MPYA KUPATIKANA

 LEO Jumamosi Julai 9,2022 Yanga itaingia kwenye historia mpya ya kumpata rais ambaye ataiongoza timu hiyo kutoka kwenye mfumo wa kuongozwa na mwenyekiti.

Yanga wanatarajia kumpata rais wa timu hiyo watakapokamilisha zoezi la uchaguzi leo Jumamosi.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere,Dar.

Mbali na kumchagua rais pia Yanga watachagua makamu wa rais pamoja na wajumbe watano.

Katika nafasi ya rais mgombea ni mmoja pekee ambaye ni Injinia Hersi Said ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya timu ya Yanga.

Kwa upande wa wagombea nafasi ya umakamu kuna majina mawili ambayo ni Arafat Haji na Suma Mwaitenda.

Rais ambaye anakwenda kuchaguliwa leo anakuwa ni wa kwanza kwenye klabu hiyo na Mshindo Msolla yeye akiwa ni mwenyekiti wa mwisho kuiongoza Yanga