HABIB Kyombo nyota aliyekuwa anakipiga ndani ya Klabu ya Mbeya Kwanza leo Julai 9 ametambulishwa ndani ya kikosi cha Simba.
Nyota huyu anakuwa ni mzawa wa kwanza kuweza kutambulishwa ndani ya kikosi hicho ambacho msimu wa 2021/22 ulikuwa ni mbaya kwao kwa kukosa kila kitu walichokuwa wanapambania.
Kombe la Shirikisho, Ngao ya Jamii na lile la ligi vyote vilikwenda mikononi mwa Yanga ambao ni watani zao wa jadi.