USIKU wa tuzo usiku wa kuamkia Julai 8/2022 umeweza kukamilika kutoka Ukumbi a Hotel ya Rotana ambapo kila aliyeweza kuchaguliwa kasepa na tuzo yake.
Miongoni mwa tuzo ambazo zilikuwa zinafuatiliwa kwa ukaribu ni pamoja na ile ya mchezaji bora pamoja na bao bora ambalo limeweza kutambuliwa ndani ya ligi msimu huu.
Tuzo hizo zimekwenda kwa mchezaji bora wa soka la ufukweni ambaye ni Adel Abdi Mohamed.
Mchezaji bora First League ni Mohamed Hussein na bao bora la msimu wa 2021/22 ni Fiston Mayele ambalo aliweza kufunga mbele ya Biashara United.
Mchezaji Bora wa Kombe la Shirikisho ni Abdul Suleiman,’Sopu’wa Coastal Union.
Mchezaji Bora Ligi ya Wanawake ni Fatuma Maono, ‘Fetty Densa’ wa Simba Queens.
Mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara ni Yannick Bangala wa Yanga.
Tuzo hizo zimefanyika katika Hotel ya Johari Rotana