LEO ni leo itakuwa kwa kuwa ni siku ya ugawaji wa tuzo kwa wanamichezo baada ya kukamilisha msimu wa 2021/22 ambapo mabingwa ni Yanga.
Julai 7 zinatarajiwa kufanyika tuzo hizo kwenye Ukumbi wa Rotana Hotel, huku moja ya kipengele ambacho kinatazwa kwa ukaribu ni upande wa mlinda mlango.
Hapa tunakuletea rekodi za mastaa hao watatu waliopenya kuwania tuzo hiyo ya kipa bora zilizoandaliwa na Bodi ya Ligi Tanzania ambapo mmoja atasepa nayo jumlajumla namna hii:-
Manula
Air Manula, Aishi Manula yeye ni kipa namba moja ndani ya kikosi cha Simba akiwa anaitetea tuzo yake ambayo alisepa nayo msimu wa 2020/21.
Msimu huu amecheza mechi 21 na kuyeyusha dk 1,890 akiwa hajafungwa kwenye mechi 11 na ametunguliwa mabao 11.
Mechi zake za ushujaa
Biashara United 0-0 Simba
Dodoma Jiji 0-1 Simba
Simba 1-0 Polisi Tanzania
Simba 0-0 Coastal Union
Simba 1-0 Namungo
Simba 0-0 Yanga
Mtibwa Sugar 0-0 Simba
Simba 1-0 Prisons
Yanga 0-0 Simba
Simba 1-0 Mbeya Kwanza
Simba 2-0Kagera Sugar
Hapa alipata tabu
Ruvu Shooting 1-3 Simba
Simba 2-1Geita Gold
KMC 1-4 Simba
Simba 2-1 Azam FC
Mbeya City 1-0 Simba
Kagera Sugar 1-0 Simba
Coastal Union 1-2 Simba
Namungo 2-2 Simba
Simba 4-1 Ruvu Shooting
Azam FC 1-1 Simba
Diarra
Kipa namba moja wa Yanga Diarra Djigui ikiwa ni msimu wake wa kwanza kuitumikia timu hiyo ambayo imesepa na ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Rekodi zinaonyesha kwamba amecheza jumla ya mechi 22 na hajafungwa kwenye mechi 15 akiwa ametunguliwa mabao 7 kwenye dk zake 1,944.
Clean sheet zake
Kagera Sugar 0-1 Yanga, dk 90
Yanga 1-0 Geita Gold,dk 90
KMC 0-2 Yanga,dk 90
Yanga 2-0 Azam FC,dk 90
Mbeya Kwanza 0-2 Yanga, dk 90
Simba 0-0 Yanga,dk 90
Mtibwa Sugar 0-2 Yanga,dk 90
Yanga 3-0 Kagera Sugar,dk 90
Geita Gold 0-1 Yanga,dk 90
Yanga 2-0 KMC,dk 90
Yanga 0-0 Simba,dk 90
Ruvu 0-0 Yanga,dk 90
Yanga 0-0 Prisons,dk 54
Dodoma Jiji 0-0 Yanga, dk 90
Yanga 4-0 Mbeya Kwanza,dk 90
Mishale ilipenya
Yanga 3-1 Ruvu Shooting,dk 90
Namungo 1-1 Yanga,dk 90
Prisons 1-2 Yanga,dk 90
Yanga 2-1 Biashara United,dk 90
Azam FC 1-2 Yanga,dk 90
Yanga 2-1 Namungo,dk 90
Mbeya City 1-1 Yanga
Aboubhakari
Khomeny Aboubhakari wa Geita Gold inayonolewa na Kocha Mkuu, Felix Minziro yeye ni miongoni mwa wanaowania tuzo hii.
Rekodi zinaonyesha kuwa ni mechi 14 ambazo amekaa langoni ambazo ni sawa na dk 1,260,hajafungwa kwenye mechi 5 na amefungwa jumla ya mabao 10 kwenye mechi 9 alizotunguliwa.