NI beki wa kulia, Nathaniel Chilambo ambaye alikuwa anakipiga ndani ya kikosi cha Ruvu Shooting amepata changamoto mpya.
Hivyo bei huyo msimu ujao wa 2022/23 atakuwa na uzi wa Azam FCpale viunga vya Azam Complex.
Chilambo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuweza kuitumikia timu hiyo ambayo inauhakika wa kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kumaliza ligi ikiwa nafasi ya 3.
Beki huyo amesaini mkataba huo mbele ya mmiliki wa timu, Yusup Bakhresa na Ofisa Mtendaji Mkuu Abdulkarim Amin wenye kipengele cha kuongeza baada ya miezi sita kutokana na kiwango atakachokionyesha.
Beki huyo mwenye miaka 19, anayetumia miguu yote miwili kwa ufasaha, mwenye uwezo pia wa kucheza beki ya kushoto, amekuwa na kiwango bora kabisa msimu uliopita