SOPU ALIYEKUWA ANATAJWA SIMBA AIBUKIA AZAM FC

BREAKING:RASMI kiungo mshambuliaji wa Coastal Union, Abdul Suleiman, ‘Sopu’ ni mali ya Azam FC.

Nyota huyo alikuwa kwenye hesabu za mabosi wa Yanga na Simba waliokuwa kwenye hesabu za kuwania saini yake.

Kwenye Kombe la Shirikisho nyota huyo kasepa na tuzo ya mchezaji bora na mfungaji bora ambapo alifunga jumla ya mabao 9 na pasi 4 alipokuwa anaitumikia Coastal Union.

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Azam FC umeweka wazi kuwa:”Tunayo furaha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba wa miaka mitatu na kiungo mshambuliaji, Abdul Sopu, akitokea Coastal Union,”.