YANGA KESHO KUIVAA COASTAL UNION

 NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa mchezo wa kesho wa hatua ya fainali dhidi ya Coastal Union utakuwa mgumu lakini wapo tayari.

Yanga inakwenda kumenyana na Coastal Union ikiwa imetwaa taji la Ligi Kuu Bara na pointi zake 74.

Imeweza kutwaa taji hilo ikiwa haijapoteza na kesho inakwenda kupambana kusaka taji lingine la kufungika msimu.

Kaze amesema:”Tumecheza na Coastal Union kwenye mechi ya ligi na tukashinda mabao 3 hivyo mchezo wetu wa fainali hautakuwa mwepesi.

“Unapozungumzia fainali huwa inakuwa sio nyepesi hasa ukweli kila timu inahitaji kushinda,tupo tayari na tutajitahidi kupata ushindi,”.

Yanga ilitinga hatua ya fainali baada ya ushindi wa bao 1-0 Simba,hatua ya nusu fainali.