MASTAA wa Simba leo Julai Mosi wamerejea Dar wakitokea Songea ambapo walikuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara kwa kufunga msimu wa 2021/22 na walicheza dhidi ya Mbeya Kwanza Uwanja wa Majimaji,Songea na kutoshana nguvu ya bila kufungana.
Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 61 baada ya kucheza mechi 30 za ligi.