UJUMBE WA BANGALA NA DJUMA KWA COASTAL UNION HUU HAPA

YANNICK Bangala na Djuma Shaban mabeki wa Yanga wameweka wazi kwamba kesho watapambana mbele ya Coastal Union kwenye mchezo wa fainali Kombe la Shirikisho.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba na kufanikiwa kutinga hatua ya fainali.

Kesho inatarajiwa kukutana na Coastal Union kwenye mchezo wa fanali ambapo mwamuzi wa kati ametangazwa kuwa Ahmed Arajiga.

Mabeki hao wameweka wazi kwamba wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini wapo tayari kupata matokeo.

“Hatujamaliza bado kazi baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kazi yetu sasa inakwenda kwenye kupambania Kombe la Shirikisho hivyo tunakwenda tukihitaji kutwaa ubingwa,” amesema Bangala.

Kwa upande wa Djuma amesema hakuna ambaye ameridhika kwa wachezaji kutwaa ubingwa wa ligi pekee hivyo wamejiandaa kushinda mechi hiyo.