RATIBA YA LIGI KUU BARA LEO

 JUNI 29,2022 Ligi Kuu Tanzania Bara ngwe ya mwisho inatarajiwa kuchezwa leo kwa kila timu kusaka pointi tatu muhimu.

Ni Mbeya Kwanza pekee ambaye ameshajua kwamba msimu jao atacheza Championship huku timu nyingine zikiwa na kazi ya kusaka ushindi kupata kile wanachopambania.

Hii hapa ratiba ya kukamilisha msimu wa 2021/22 ambapo bingwa ni Yanga amecheza mechi 29 bila kufungwa.

Mbeya Kwanza v Simba, Uwanja wa Majimaji, Songea

Dodoma Jiji v KMC, Uwanja wa Jamhuri,Dodoma

Yanga v Mtibwa Sugar Uwanja wa Mkapa

Ruvu Shooting v Prisons, Uwanja wa Mabatini

Kagera v Polisi Tanzania, Uwanja wa Kaitaba

Mbeya City v Namungo, Uwanja wa Sokoine

Coastal Union v Geita, Uwanja wa Mkwakwani

Azam FC v Biashara United, Uwanja wa Azam Complex.

Mechi zote kuchezwa saa 10:00 jioni.