GEITA GOLD YAFUNGIWA NA FIFA KUSAJILI

SHIRIKISHO la Kimataifa la Soka (FIFA) limeifungia Klabu ya Geita Gold kusajili wachezaji hadi itakapomlipa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Ettiene Ndayiragije.

Kocha huyo raia wa Burundi alifungua madai dhidi ya Geita Gold akidai fidia ya kuvunjiwa mkataba pamoja na malipo mengine wakati akiifundisha timu hiyo ya mkoani Geita.

Kwa mujibu wa taratibu za FIFA, iwapo Geita itakuwa haijamlipa kocha huyo suala hilo litawasilishwa katika Kamati ya Nidhamu ya FIFA kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu.

Taarifa ambayo imetolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)imeweka bayana kwa  kuzikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zinaingia na wachezaji pamoja na makocha, kwani hiyo ni moja ya vigezo vya kupata Leseni ikiwa ni utekelezaji wa Kanuni ya Leseni za Klabu (Club Licensing Regulations).

Kwa sasa Geita Gold ipo chini ya Felix Minziro ambaye anakinoa kikosi hicho chenye mzawa namba moja kwa utupiaji ambaye ni George Mpole mwenye mabao 16.