WAWA AAGWA SIMBA KWA USHINDI UWANJA WA MKAPA

BEKI kisiki wa Simba, jana Juni 23 2022 aliagwa rasmi kwenye kikosi hicho kwa kushuhudia ushindi wa mabao 2-0 kwa timu hiyo ambayo inacheza Ligi Kuu Bara.

Ni mabao ya Pape Sakho dk ya 17 na Peter Banda dk ya 44 yalitosha kuipa pointi tatu Simba, kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Wawa ambaye amedumu kwa misimu minne mabosi wa Simba wamesema kwamba hawatamuongezea mkataba kwa msimu ujao hivyo atakuwa mchezaji huru.

Beki huyo alionyesha uwezo mkubwa na kufanya kazi kubwa kuweka lango la Beno Kakolanya kwenye mikono salama.

Licha ya makosa ambayo yalikuwa yanatokea kwenye kipindi cha kwanza kushindwa kuwa na maelewano mwanzo wa mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Simba inafikisha pointi 60 ikiwa nafasi ya pili na Mtibwa Sugar ikiwa nafasi ya 12 na pointi 31 na timu zote zimecheza mechi 28.

Kwenye mchezo huo nyota wa Mtibwa Sugar,Said Ndemla aliweza kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea faulo Sadio Kanoute.