IKIWA imefanikisha lengo la kufuzu kushiriki Kombe la Dunia kwenye Kombe la Dunia kwa timu ya Wasichana ya Tanzania, U 17, Serengeti Girls kundi lao ni D.
Timu hiyo imefanikisha malengo hayo kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1 Cameroon ulioifanya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Bakari Shime kukamilisha lengo hilo Juni 5,mwaka huu.
Michuano hiyo inatarajiwa kufanyika India Oktoba 2022.
Kwenye kundi D itakuwa na timu nyingine ambazo ni Japan,Canada na Ufaransa