NYOTA wa Biashara United, Ramadhan Chombo ‘Redondo’ ameweka wazi kuwa msimu ujao atakuwa nje ya Biashara United ambayo anaitumikia kwa sasa.
Ikumbukwe kwamba nyota huyo amebakiza mechi mbili tu kuvua rasmi jezi ya timu hiyo baada ya kuivaa kwa misimu mitatu na msimu ujao hatakuwa katika kikosi hicho.
Licha ya kushindwa kuweka wazi, atakuwa timu ipi, Redondo ameweka wazi kwamba mkataba wake na Biashara unameguka mwisho wa msimu huu na hataendelea nao.
“Msimu ujao nitakuwa timu nyingine, tuombe uzima tu. siwezi kutaja timu kwa sasa kwani bado nipo Biashara na ligi hajiamalizika, ila baada ya msimu kuisha itakuwa wazi,” amesema Redondo.
Biashara United inapambana na hali yake kwa sasa ili kuweza kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao.
Ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 25 baada ya kucheza mechi 28.