NGOMA NZITO KAITABA WAGAWANA POINTI MOJAMOJA

DAKIKA 90 zilikuwa nzito kwa Kagera Sugar dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wa ligi baada ya kugawana pointi mojamoja.

Ilikuwa ni Uwanja wa Kaitaba ambapo mchezo huo wa ligi ulichezwa Juni 18, 2022 kwenye msako wa pointi tatu kila timu iliambulia moja.

Ni bao la Wazir Junior lilikuwa la kwanza kupachikwa kimiani dk ya 60 kisha lile la Dodoma Jiji ilikuwa ni dk ya 83 kwa mkwaju wa penalti mtupiaji akiwa ni Abeid Athuman.

Sasa Dodoma Jiji inafikisha pointi 32 nafasi ya 11 huku Kagera Sugar ikiwa na pointi 35 nafasi ya 7 kwenye msimamo.

Mabingwa ni Yanga ambao walitangazwa kuwa mabingwa baada ya ushindi wa mabao 3-0 Coastal Union