MAYELE ANACHOFIKIRIA KUHUSU UFUNGAJI BORA KIPO HIVI

 FISTON Mayele mshambuliaji namba moja wa Yanga amesema kuwa kwa sasa hafikirii suala la tuzo ya kiatu cha ufungaji bora zaidi ya kuweza kutimiza majukumu yake.

Mayele katupia mabao 16 kwenye ligi aaongoza ndani ya kikosi cha Yanga akiwa ni mchezaji mgeni mwenye mabao mengi msimu huu.

Idadi hiyo ya mabao imefikiwa pia na mzawa George Mpole ambaye yeye ni mzawa anacheza ndani ya kikosi cha Geita Gold kinachonolewa na Kocha Mkuu, Felix Minziro.

Mayele amesema;”Ligi imekuwa na ushindani mkubwa na kila mchezaji anafanya vizuri kupata matokeo kwangu mimi naona kwa kila mchezaji ana kazi ya kutimiza majukumu yake suala la kufikiria kiatu cha ufungaji hilo itakuwa baadaye.

“Kwanza ni ushindi na ninafurahi kuona kwamba tumetwaa ubingwa na kazi ambayo imebaki kwa mechi zijazo ni kuweza kuendelea kushinda kwa ajili ya pointi tatu muhimu,” amesema.

Mchezo ujao wa Yanga ni dhidi ya Polisi Tanzania unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa itakuwa ni Juni 22 ambapo utakuwa ni mchezo wa mwisho msimu huu wa ligi Yanga kucheza kwenye uwanja huo.