SIMBA KUYAKOSA MABAO 8 LIGI KUU BARA

MASTAA watatu wa Simba ambao wamehusika kwenye mabao 8 kati ya 33 wanatarajiwa kuukosa mchezo wa leo dhidi ya Mbeya City, Uwanja wa Mkapa.

Ni John Bocco mwenye mabao 3 Jonas Mkude mwenye pasi mbili za mabao na Clataous Chama mwenye mabao matatu hawa jana na juzi walipewa program maaalumu kwa ajili ya kuwarejesha kwenye ubora wao.

Mkude ambaye ni kiungo aliumia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa Uwanja wa Mkapa huku Chama yeye akipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Yanga.

Kwa upande wa nahodha Bocco alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Geita Gold ambao ulichezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Katika mazoezi ya jana ambayo yamefanyika katika Uwanja wa Simba Mo Arena nyota hao watatu chini ya Seleman Matola walikuwa wakifanya mazoezi yao tofauti na wengine.

Huenda wakaukosa mchezo wa leo dhidi ya Mbeya City ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ukiwa ni wa mzunguko wa pili baada ya ule wa awali Simba kupoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Matola amesema kuwa kuhusu wachezaji amao watacheza leo inategemea ripoti ya daktari.

“Tunajua kwamba wapo wachezaji ambao hawajawa fiti lakini wameanza mazoezi hivyo ambacho tunakifanya kwa sasa ni kusubiri ripoti ya daktari,”.