HAJI MANARA ATEMA NYONGO BAADA YA YANGA KUBEBA UBINGWA – VIDEO

Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amesema Rais mtarajiwa wa klabu hiyo Injinia Hersi Said ndiyo mwamba aliyeleta mafanikio makubwa ndani ya klabu hiyo kutoka na kujitoa kwake kuipambania Yanga katika kila hatua.

Manara amemmwagia Hersi sifa hizo wakati akiongea na waandishi wa habari katika mkutano wake ambao ameupa jina la Mkutano wa kuhutubia Taifa hii ikiwa ni mara baada ya jana klabu ya Yanga kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa 2021/2022.

Mbali na Hersi Manara pia amemshukuru Mfadhiri/Mdhamini wa klabu hiyo Ghalib Said Mohamed (GSM) kwa namna anavyojitoa katika kuisaidia klabu hiyo, sambamba na huyo amewapongeza wachezaji pamoja na benchi zima la ufundi kwa kufanikisha kuisaidia timu hiyo kuchukua kombe la 28 la Ligi kuu Bara.