AZAM FC imewashusha Geita Gold kwenye nafasi ya tatu baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya Kwanza.
Mchezo huo ulichezwa katika Uwanja wa Azam Complex na ulikuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa Mbeya Kwanza wanapambana kushuka daraja.
Ni mabao ya Shabaan Chilunda dk ya 45+1 na Idris Mbombo aliyepachika bao hilo dk ya 83.
Sasa Azam FC inafikisha pointi 40 huku wakiishusha Geita Gold kwenye nafasi hiyo ikiwa nafasi ya nne na pointi zao ni 39.
Tayari mabingwa washajulikana ambao ni Yanga wao walishinda mabao 3-0 Coastal Union, Uwanja wa Mkapa.
Mbeya Kwanza ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 24 kibindoni.