UJENZI WA UWANJA WA SIMBA MAMBO YAZIDI KUPAMBA MOTO

MTENDAJI Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa leo wameongozana na msanifu majengo (architect) kwa ajili ya kutembelea eneo la Bunju ili kukagua mipaka na eneo ambalo litatumika kwenye ujenzi kabla ya Ijumaa Bodi ya Wakurugenzi Simba kukutan.

Kwa mujibu wa Barbara ni kwamba lengo la kuweza kukutana Ijumaani kuweza kumpitisha mkandarasi ambaye atasimamia ujenzi pamoja na kupitia, proposal (kazi mradi) iliyoandaliwa.

Barbara amesema:”Tumeweza kutembelea katika eneo hili la Bunju na mchora michoro ambapo kazi ya kwanza ilikuwa ni kuweza kuona namna eneo lilivyo pamoja na namna ya kuweza kukamilisha ile kazi ya michoro.

“Ili uweze kujenga uwanja ni lazima ujue unahitaji kuwa na sehemu kubwa pamoja na sehemu ya kuweza kuwa na vitu vyote vya muhimu vinavyohitajika kwenye ujenzi wa uwanja.

“Hiyo ni pamoja na GYM,sehemu ya kukaa vijana,sehemu ya kukaa kwa timu mwenyeji na mgeni, pia benchi la ufundi nalo linapaswa kuwa na ofisi zake haya yote ni lazima tuwe nayo na nilipewa proposal na Bodi ya Wakurugenzi kwamba lazima tutafute yale ambayo yanahitajika.

“Ijumaa Bodi itakaa kwa kuwa wao wana uzoefu kuhusu masuala ya ujenzi wa viwanja na wametembelea viwanja mbalimbali duniani hapo itakuwa ni kazi ya kuweza kuangalia na kuboresha kwa yale ambayo nitakuwa nimependekeza.

“Pia kuna suala la ujenzi wa viwanja vya nyasi asili ambazo hizo zinatumika sehemu nyingi duniani hivyo nguvu kubwa itakuwa kwenye ujenzi wa viwanja vya nyasi  asili ambapo tunataka kuwa navyo vitatu na wa nyasi bandia mmoja,” amesema Barbara.