USHINDI wa mabao 3-1 waliopata Mtibwa Sugar unawapandisha kwa hatua moja kutoka nafasi ya 12 waliyokuwa mpaka ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.
Wakati Mtibwa Sugar wakiwa kwenye furaha mashabiki wa Ruvu Shooting wao wapo kwenye huzuni kwa sababu timu yao imeganda palepale ilipokuwa nafasi ya 13 na pointi zao ni 28.
Mabao ya Mtibwa Sugar yalifungwa na Brian Mayanja aliyeweza kutupia mabao mawili ilikuwa dk ya 56 na 75 huku lile la kwanza likiwa ni la kujifunga kwa Kombo dk ya 41.
Ruvu Shooting walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa kiungo wao Abalkassim ilikuwa dk ya 86 kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Manungu.