LIGI Kuu Tanzania Bara leo Juni 14 inaendelea ambapo kuna mechi mbili zitachezwa kwenye viwanja tofauti.
Ni KMC yenye pointi 31 baada ya kucheza mechi 25 hii itamenyana na Tanzania Prisons yenye pointi 25 aada ya kucheza mechi 26.
Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru.
Pia mchezo mwingine ni ule wa Kagera Sugar yenye pointi 33 baada ya kucheza mechi 26 na watapambana na Biashara United yenye pointi 24.
Huu ni mzunguko wa pili wa ligi ambapo mpaka sasa bado hazijajulikana timu ambazo zinatarajiwa kushuka ila zile zilizopanda zikiwa zinajulikana ni Ihefu na DTB.