STAA wa Geita Gold, mzawa George Mpole kafikisha jumla ya mabao 15 ndani ya ligi akiwa ni namba moja kwa utupiaji kwa sasa.
Bao la 15 alifunga mbele ya Dodoma Jiji ilikuwa dk ya 77 wakati timu hiyo iliposhinda mabao 2-0 Uwanja wa Nyankumbu jana.
Anayefuata kwenye suala la utupiaji ndani ya ligi ni Fiston Mayele wa Yanga mwenye mabao 14 na pasi tatu za mabao.
Geita Gold kwenye msimamo ipo nafasi ya 3 Geita ikiwa na pointi 39 baada ya kucheza mechi 27.
Wamewashusha kwenye nafasi ya 3 Namungo FC ambayo ina pointi 37 baada ya kucheza mechi 26.