YANGA YADAIWA KUMSAJILI KAMBOLE WA KEIZER CHIEF

Klabu Yanga imeripotiwa kushinda mbio za kuinasa saini ya mshambuliaji wa Keizer Chiefs Lazarous Kambole (28) kwa mkataba wa miezi 6 wenye chaguo la nyongeza ya miaka miwili.

Yanga SC imeipiku klabu ya Zesco United katika mbio za mshambuliaji huyo raia wa Zambia ambaye amefunga magoli mawili tu katika mechi 46 kwa kipindi cha miaka miwili alichokuwa klabuni hapo.