ARTETA AHOFIA KUMKOSA JESUS… HABARI MBAYA KWA MASHABIKI WA ARSENAL

LONDON, England

BOSI wa Arsenal, Mikel Arteta, amekasirishwa na kitendo cha klabu hiyo kuonekana kusuasua katika maamuzi ya usajili, huku akiwa na hofu huenda akamkosa Gabriel Jesus ambaye ni muhimu kwake.

Arteta alitumia pauni 150m katika usajili uliopita akimsajili Ben White, Aaron Ramsdale na Martin Odegaard.

Kuelekea msimu ujao wa 2022/23, Arsenal inajipanga kuona inaimarisha zaidi kikosi chake ambapo kinatarajiwa kushiriki Europa League.

Arteta kwa sasa anataka kusajili straika akimuhitaji Jesus. Nafasi zingine anazotaka kusajili ni kiungo na beki.

Kocha huyo aliwahi kufanya kazi na Jesus kwenye kikosi cha Manchester City akiwa msaidizi wa Pep Guardiola, hivyo inaaminika huenda akafanikiwa kukamilisha dili hilo.

Nyota huyo atatua hapo kuziba nafasi ya Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette walioondoka kwa nyakati tofauti msimu wa 2021/22.

Hofu kubwa kwa Arteta ni kumkosa Jesus ambaye dau lake ni pauni 50m.

Imeelezwa Arteta anapata ugumu kwani safari hii masuala ya fedha ni lazima yapitie kwa mmiliki wa klabu, hivyo kocha huyo anaweza kuwakosa nyota muhimu ambao anaowahitaji.

Wakati Arsenal wakiwa bize na Jesus, Chelsea na Tottenham nao wanatajwa kuwa katika dili hilo.

Arsenal ilimaliza nafasi ya tano ndani ya Premier League msimu wa 2021/22.