AZIZ KI USO KWA USO NA INJINIA HERSI,SIMBA KUAMBULIA PATUPU

 ISHU ya kiungo wa ASEC Mimosas Aziz KI imezidi kuleta ugumu kwa vigogo wa Dar ambapo Yanga na Simba wanaonekana kuhitaji saini yake.

Ni Simba walianza kumvutia kasi kiungo huyo ambaye aliwatungua kwenye mashindano ya kimataifa kisha vinara wa ligi Yanga nao wakaanza kumvutia kasi.

Inaelezwa kuwa mabosi wa Yanga wamewazidi ujanja Simba kwa kuweza kumalizana na kiungo huyo kwa dili la miaka miwili ambalo alikuwa anatajwa kwamba alisaini ndani ya kikosi cha Simba.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Simba kuna barua ambayo ilikuwa inaeleza kwamba nyota Aziz Ki amesaini dili la miaka miwili ambapo kulikuwa na saini ya Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez, barua hiyo ilikuwa inasambaa mtandaoni imefafanuliwa kuwa sio halisi.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga ameachia picha kwenye mtandao wake wa kijamii ikimuonyesha Injinia Hersi Said akiwa na mchezaji huyo wakipata chakula na kudondosha maneno kuwa wakibisha ataonyesha picha za mkataba.

Kwa picha hilo inaonyesha kuwa kiungo huyo amemalizana na Yanga ni suala la muda tu huku Simba wakiambulia patupu.