WINGA HUYU WA KAZI AWEKWA RADA ZA YANGA

IMEELEZWA kuwa mabosi wa Yanga wanamtazama kwa ukaribu kiungo wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Aziz Ki ili waweze kupata saini yake.

Nyota huyo pia anatajwa kuingia kwenye rada za Simba ambao nao pia wanahitaji kumpata kwa ajili ya msimu mpya.

Nyota huyo ni raia wa Burkina Faso aliweza kufanya vizuri akiwa na timu yake kwenye mechi ambazo walikuwa wanacheza kwenye mashindano ya kimataifa.

Habari zinaeleza kuwa Aziz alianza mazungumzo muda mrefu na mabosi wa Yanga ambao wapo kwenye hatua ya kuweza kuinasa saini yake.

Pia uwepo wa Yacouba Songne ambaye ni raia wa Burkina Faso unatajwa kuongeza nguvu ya kiungo huyo kuweza kusaini dili jipya ndani ya Yanga.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela hivi karibuni alisema kuwa wapo wangi ambao wapo kwenye mazungumzo na Yanga ikifika wakati taarifa itatolewa.