WACHEZAJI WAPIGWA MKWARA NA NABI

NASREDDINE Nabi,Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake bado wana kazi ya kufanya kwa ajili ya mechi zilizobaki na kufikia malengo ya kutwaa ubingwa wa ligi.

Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 64 baada ya kucheza 26 na haijapoteza mchezo hata mmoja.

Nabi amesema kuwa licha ya kuwaacha wapinzani wao Simba kwa pointi 13 bado wana kazi kubwa ya kufanya kwa ajili ya kukamilisha mzunguko wa 2021/22.

“Bado wachezaji wana kazi ya kufanya kwa ajili ya mzunguko wa pili na kukamilisha mechi ambazo zipo kwani bado kazi inaendelea hasa kwa kuweza kupata ushindi zaidi.

“Uzuri ni kwamba kila mchezaji anajua majukumu yake na kwa hapa ambapo tupo hatujafikia malengo yale tuliyojiwekea hasa kwa kuweza kushinda kile ambacho tunakihitaji na kazi bado ipo,”.

Kwenye Kombe la Shirikisho, Yanga imetinga hatua ya nusu fainali na inatarajiwa kucheza na Coastal Union kwenye mchezo wa fainali.