PROFESSOR JAY ARUHUSIWA HOSPITALI

MWANAMUZIKI maarufu wa Hip Hop nchini na mbunge mstaafu wa Mikumi, Joseph Haule (Prof. Jay) aliruhusiwa kurejea nyumbani Juni 9, 2022 kutoka hospitali alikokuwa amelazwa baada ya kupatiwa matibabu kwa siku 127 na afya yake kuimarika.

Leo Juni 10 Hospitali ya Taifa Muhimbili imeeleza taarifa hiyo kupitia kwenye mtandao wake wa kijamii.

Nyota huyo aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Mikumi ni miongoni mwa mastaa ambao wanafanya vizuri kwenye masuala ya utunzi na uimbaji pia.