NYOTA wa kikosi cha Azam FC, Ibrahim Ajibu ameweza kurejea katika kikosi hicho hivyo anatarajiwa kuwa miongoni mwa wale watakaoonyesha makeke kwa mechi zijazo.
Ingizo hilo jipya ndani ya Azam FC msimu huu liliibuka hapo kutokea ndani ya Simba na halijawa kwenye mwendo mzuri.
Sababu kubwa za kukosekana kwenye kikosi hicho ni matatizo ya kifamilia jambo ambalo limemfanya asiwe kwenye mechi za ligi.
Ajibu alikosekana kwenye mechi tatu ilikuwa miwili ya ligi ilikuwa dhidi ya Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar na mchezo mmoja ulikuwa mbele ya Coastal Union huu ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho,
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa tayari Ajibu amejiunga na kikosi hicho aada ya kumaliza matatizo ya kifamilia.