FELIX Minziro, Kocha Mkuu wa Geita Gold amesema kuwa wanahitaji kumaliza ligi ndani ya tano bora hivyo wataendelea kupambana kufanikisha malengo yao.
Mchezo uliopita ubao wa Uwanja wa Sokoine, ulisoma Tanzania Prisons 1-1 Geita kwa mabao ya Jeremia Juma dk ya 38 na Danny Lyanga dk ya 50.
Minziro amesema kuwa kila wanapomaliza mchezo ni mwanzo wa kujiandaa kwa ajili ya mchezo wao ujao ambao wanaupa umuhimu.
“Kila baada ya mchezo tunayafanyia kazi makosa yetu ili kuweza kuwa imara kwa mchezo unaokuja na malengo yetu ni kuona kwamba tunakuwa ndani ya tano bora.
“Haitakuwa kazi rahisi kwani kila timu inahitaji ushindi lakini ambacho tunapaswa kufanya ni kuendelea kutafuta ushindi kwenye mechi ambazo tutacheza,” alisema Minziro.
Geita Gold ipo nafasi ya 5 ikiwa na pointi 36 baada ya kucheza mechi 26.
Mtupiaji wao namba moja ni George Mpole mwenye mabao 14 ndani ya ligi.