COASTAL UNION YATINGA HATUA YA FAINALI,KOMBE LA SHIRIKISHO

 COASTAL Union ya Tanga leo Mei 29 imekata tiketi ya kutinga hatua ya fainali Kombe la Shirikisho kwa ushindi mbele ya Azam FC.

Ilikuwa dakika 120 za kazi kwa kuwa dk 90 ubao ulisoma Coastal 0-0 Azam FC, na hata zilipoongezwa 30 kukamilisha 120 bado ngoma ilikuwa ni ngumu kwa timu zote.

Mshindi amepatikana kwa mikwaju ya penalti Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambaye ni Coastal Union kwa penalti 6-5 Azam FC.

Sasa fainali itakuwa ni Yanga v Coastal Union, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Julai 2.

Mpigaji penalti wa kwanza kwa Azam FC alikuwa ni Lusajo Mwaikenda na penalti yake iliokolewa na Mohamed Hussein na kwa Coastal Union ni Miraj Adam huyu alikosa penalti baada ya kupaisha.