AZAM FC YAWAITA MASHABIKI ARUSHA

 ZAKARIA Thabit, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa kwa sasa mashabiki wa Azam FC wana kazi moja tu kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuweza kushuhudia burudani.

Azam FC leo Mei 29 itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Coastal Union kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.

Mshindi wa mchezo wa leo anakwenda kukutana na Yanga iliyokata tiketi ya kutinga hatua hii kwa ushindi wa bao 1-0 Simba, kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Thabit amesema:”Mashabiki wa Azam FC tukutane Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa ajili ya mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Coastal Union.

“Tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu lakini tupo tayari kwa ajili ya ushindani kwa maandalizi ambayo tumefanya tunaamini kwamba  tutapata matokeo hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi,”.