YANGA YABAINISHA WAMEUKAMATA MCHEZO DHIDI YA SIMBA

KOCHA Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema wameukamata vizuri mchezo wa nusu fainali Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba utakaochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Ni leo Mei 28 mchezo huo ambao umeshika hisia za mashabiki wengi unatarajiwa kuchezwa kwa timu ambayo itatinga hatua ya fainali.

Mshindi wa mchezo wa leo anatarajiwa kucheza na mshindi wa Coastal Union v Azam FC ambao utachezwa kesho, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwenye fainali.

Nabi amesema: “Tumeukamata vizuri mchezo wa leo na tunajua kwamba wapinzani wetu wapo vizuri kwa kuwa wameweza kufika hapa hivyo tunawaheshimu.

“Kila mchezaji yupo tayari na tunaamini utakuwa mchezo mzuri, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuweza kuona namna gani tutatoa burudani kwenye mchezo wetu,”.

Mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho ni Simba ambao walitwaa taji hili mbele ya Yanga kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika.