IMEELEZWA kuwa kipa namba mbili wa Simba, Beno Kakolanya ameandaliwa kubeba mikoba ya Aishi Manula kwenye mchezo wa leo hatua ya nusu fainali.
Simba ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Yanga kwenye mchezo ambao unaotarajiwa kuchezwa leo Uwanja wa CCM Kirumba.
Taarifa zimeeleza kuwa Manula yeye alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Geita Gold baada ya kukwata na vioo muda mfupi kabla ya mechi kuanza.
Mkuu wa Idara ya Habari ndani ya kikosi cha Simba, Ahmed Ally amesema kuwa Manula tupo vizuri na ameanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wa leo.
“Manula yupo vizuri kwa kuwa alipata maumivu na sasa yupo vizuri kwa ajili ya mechi yetu dhidi ya Yanga,”