JEMBE:AMBUNDO ANAJAMBO KUBWA LA KUJUTIA KULIKO SAIDO

MCHAMBUZI mwandamizi wa michezo nchini Saleh Ally ‘Jembe’ amesema kuwa mchezaji wa Yanga, Dickson Ambundo anatakiwa kujitafakari zaidi pengine kuliko hata mchezaji mwenzake Saido Ntibazonkiza ambao wote wamesimamishwa na Yanga kwa kosa la kutoroka kambini.

Ambundo ni mchezaji mzawa ambaye amepita katika vilabu kadhaa kabla ya kutua Yanga ikiwemo Gor Mahia ya Kenya pamoja na Dodoma Jiji, hivi karibuni mara baada ya mchezo wa Yanga dhidi ya Biashara United taarifa ziliibuka za nyota hao wawili kusimamishwa na Klabu ya Yanga kutokana na kosa la kutoroka kambini.

Kwa nafasi yake kama mchambuzi mkongwe wa soka nchini Jembe amedai kuwa kwa namna yoyote ile Ambundo ndiye anaonekana mjinga katika hilo sakata kwa sababu yeye ndiyo kwanza bado ana umri mdogo hawezi kumuiga tabia Saido.

Amebainisha kwamba Saido yeye ameshacheza hadi Ulaya tena si kwa bahati mbaya ni kwa uwezo kwa hiyo Saido ana mafanikio makubwa kuliko yeye na pengine anaelekea mwisho wa maisha yake ya soka kwa kiasi kikubwa hana cha kupoteza.

“Kati ya hao we unamuona nani hana akili vizuri.”? Alihoji Jembe.

“Mdogo ndiyo hana akili vizuri, wewe una kazi ndefu ya kufikia alipofikia mwenzako, Saido kashatoka kacheza Ulaya, unajua kabisa huyu ndugu yangu baada ya muda mfupi anaanza kugombania NSSF zake dirishani, wewe inakuwaje ndiyo unaanza kupump unakuja juu unakubali vipi akuondoe?

Yanga na Simba zinatarajia kumenyana katika Uwanja wa CCM Kirumba Jumamosi hii ya Mei 28 katika hatua ya nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.