CHEZA KWA 1000 UPATE BILIONI 1 YA SUPA JACKPOT SPORTPESA

KAMPUNI ya Michezo na Burudani SportPesa  imezindua rasmi Jackpot mpya inayoitwa Supa Jackpot kama moja ya huduma yao nyingine kwa wachezaji wake.

Akizungumza ofisini kwake, Oysterbay, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tarimba Abbas amesema ni siku nyingine ambayo Kampuni ya SportPesa inatambulisha huduma hiyo.

‘’Najua bado watu wanashauku na Jackpot yetu ambayo imeliwa siku si nyingi zilizopita, kwa muktadha huo baada ya kuona wachezaji wetu wameanza kuzoea viwango vikubwa basi tumeonelea tuwaletee bidhaa ambayo inaendana na matamanio yao. Kwa hivyo tunazindua rasmi Jackpot hii ambayo itaanzia bilioni moja na itaenda kwa jina la SUPA JACKPOT’.

Tarimba amesema Supa Jackpot itakuwa na jumla ya timu 17 na pia kiwango cha pesa ambacho mchezaji atatakiwa kuweka ni Tsh 1000 ili aweze kucheza.

Lakini upekee wa Jackpot hii upo kama ifuatavyo. Jackpot imegawanyika katika makundi au vipengele vitano vya zawadi ambavyo vyote mchezaji anachaguo la kushiriki na kushinda.

Kipengele namba moja ni cha timu 17 ambacho ukishinda unaondoka na kuanzia bilioni 1 kutegemeana na Jackpot imesimamia kiasi gani. Kipengele hiki bonasi zake zinaanzia timu 16 mpaka 12.

Kundi la pili au Kipengele namba 2 ni cha timu 16 ambacho ukipatia mechi zote unashinda kuanzia Tshs milioni 750. Kipengele hiki bonasi zake zinaanzia timu 15 mpaka mechi 11.

Kundi la tatu au kipengele namba tatu ni cha timu 15 ambacho ukipatia mechi zote kwa usahihi unashinda kuanzia Tshs milioni 500. Kipengele hiki bonasi zake zinaanzia mechi 14 mpaka mechi 10

Kipengele cha nne cha Supa Jackpot ni cha timu 14 ambacho ukipatia mechi zote kwa usahihi utashinda kuanzia Tshs milioni 300. Kipengele hiki bonasi zake zinaanzia timu 13 mpaka timu 10

Na kipengele cha mwisho hichi ni kipengele ambacho kimezoeleka kila siku ni cha timu 13 ambacho ukipatia kwa usahihi unashinda kuanzia Tsh mil 200