IMEELEZWA kuwa nyota wawili ndani ya kikosi cha Yanga wametimuliwa kambini kutokana na kushindwa kufuata utaratibu ambao upo.
Ni winga Dickosn Ambundo ambaye amekuwa kwenye mwendo mzuri kwenye mechi za hivi karibuni kwa kuwa chaguo la kwanza kwa Kocha Mkuu,Nasreddine Nabi.
Pia nyota mwingine ni Said Ntibanzokiza ambaye yeye ni kiungo mshambuliaji.
Habari zimeeleza kuwa sababu ya kuweza kuondolewa kambini ni kuondoka bila kupewa ruhusa.
Kutokana na jambo hilo huenda wasiwe sehemu ya kikosi cha Yanga ambacho kitavaana na Simba kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Mei 28,2022 Uwanja wa CCM Kirumba.
Chanzo:Spoti Xtra.