IHEFU WAKABIDHIWA UBINGWA WA CHAMPIONSHIP

KLABU ya Ihefu imekabidhiwa Kombe lao la ubingwa wa Championship baada ya kumalizika kwa mchezo maalumu dhidi ya DTB uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Katika mchezo huo uliochezwa jana Mei 24, DTB iliweza kushinda bao 1-0 lakini haikuweza kutibua furaha ya mabingwa hao wanaonlewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila.

Timu zote mbili zitashiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23 baada ya kuweza kupanda daraja.

Ihefu ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 66 sawa na DTB ila tofauti yao ilikuwa ni kwenye idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Ihefu ilikuwa imefunga jumla ya mabao 50 huku DTB ikiwa imefunga mabao 44.