LEO Mei 24 Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wasichana U 17 Serengeti Girls baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Amaan Abeid Karume, Zanzibar wakitokea Cameroon walikokwenda kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Cameroon.
U 17 waliweza kupeperusha vema Bendara ya Tanzania ambapo walipata ushindi wa mabao 4-1 katika mchezo huo wa mkondo wa kwanza hivyo wana kazi ya kufanya kwenye mchezo wa pili wa marudio.
Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ambapo wanahitaji sare ama ushindi ili kuweza kufuzu Kombe la Dunia.
Kwa mujibu kwa Kocha Mkuu, Bakari Shime amesema kuwa bado kazi inaendelea kwa kuwa malengo ni kupata ushindi kwenye mchezo ujao.
“Tutakuwa na kazi kubwa na bado hatujakamilisha kazi yetu mpaka pale tutakapopata nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia inawezekana,” amesema.