MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar umeshamalika hivyo wameanza safari ya kurejea Dar.
Jana Ruvu Shooting ilitoshana nguvu bila kufungana na Kagera Sugar kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Kagera Sugar 0-0 Ruvu Shooting na kuwafanya wagawane pointi mojamoja ndani ya ligi.
Bwire ameweka wazi kwamba kwa sasa wapo safarini kurejea Pwani baada ya kumaliza mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar.
“Tumemaliza mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar na sasa tumetoka Bukoba tupo njiani kuelekea Pwani, hivyo matokeo ya mchezo wetu yameshapita na hatuwezi kuzungumzia maandalizi ya mchezo ujao kwa kuwa tupo safarini,” amesema.
Kwa mujibu wa ratiba inaonyesha kwamba Mei 24,2022 Ruvu Shooting ina kibarua cha kumenyana na Azam FC kwenye mchezo unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mabatini.
Safari iwe njema wachezaji na familia ya michezo, Ruvu Shooting