MAYELE AITAJA PASI YA SURE BOY KUWA NI YA VIWANGO

FISTON Mayele mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Yanga akiwa ametupia mabao 13 na pasi tatu amesema kuwa pasi ya kiungo Salum Aboubhakari, ‘Sure Boy’ ni ya viwango vikubwa.

Mayele hakufunga kwenye mechi nne mfululizo za ligi na mara ya mwisho kufunga ilikuwa mbele ya Namungo FC kwenye ushindi wa mabao 2-1.

Alifunga bao lake la 13 kwenye mchezo dhidi ya Mbeya Kwanza kwa pasi ya Sure Boy Uwanja wa Mkapa waliposhinda mabao 4-0.

Mayele amesema kuwa moja ya pasi nzuri na za viwango bora ni pamoja na aliyopewa na Sure Boy kwenye mchezo dhidi ya Mbeya Kwanza.

“Ile sijui niseme nini moja ya pasi za viwango ambazo huwa tunafanyia mazoezi na nimefurahi kufunga kwa kuwa nilipita kwenye muda bila kufunga hivyo nitazidi kupambana zaidi kwenye mechi zijazo na ninamshukuru Sure kwa pasi nzuri,”.

Mchezo ujao wa Yanga ni dhidi ya Biashara United unatarajiwa kuchezwa kesho Mei 23, Uwanja wa CCM Kirumba,Mwanza.