DAKIKA 90 zimekamilika Uwanja wa CCM Kirumba kwa timu zote kugawana pointi mojamoja za ligi.
Ni bao la George Mpole dk ya 20 na Kibu Dennis dk ya 27 kwa pasi ya Rally Bwalya kwenye mchezo wa leo ambao ulikuwa ni wazi kwamba kila timu ilikuwa na nafasi ya kushinda.
Sasa Mpole anafikisha mabao 14 kwenye ligi na Kibu anafikisha mabao 7 kwenye ligi ndani ya kikosi cha Simba.
Felix Minziro, Kocha Mkuu wa Geita Gold amesema kuwa ulikuwa ni mchezo ambao walikuwa wanastahili kushinda ila nafasi walishindwa kuzitumia.
“Tulitengeneza nafasi nyingi kwenye mchezo ila tumeshindwa kuzituumia kutokana na wachezaji kutokuwa makini hasa kwenye umaliziaji.
“Tulikuwa tunacheza na timu nzuri na yenye wachezaji wazuri mwisho tumepoteza pointi mbili kwenye mchezo wetu wa leo,” amesema.