MABINGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA RS BERKANE

 KLABU ya RS Berkane ya Morroco ni mabingwa wapya wa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kushinda kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Sare ya kufungana bao 1-1 iliwafanya waweze kufika hatua ya kupigiana penalti ambapo RS Berkane ilishinda kwa penalti 5-4 za Orlando Pirates.

Dakika 90 za awali zilikamilika kwa wababe hao ambao walikuwa kundi moja na Simba bila kufungana na kwenye dakika 30 za nyongeza hapo mabao yaliweza kupatikana.

Rekodi zinaonyesha kwamba Orlando Pirates walipiga jumla ya mashuti 12 na RS Berkane timu aliyokuwa anacheza Clatous Chama walipiga mashuti 8.

Fainali hiyo ilichezwa Uwanja wa Godswill Akpabio ulikuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa timu zote zilikuwa zinahitaji kombe hilo kubwa Afrika.

Bao la RS Berkane lilifungwa na Thembonkosi dk 117 na lile la Orlando Pirates lilifungwa na Youssef El Fahil dk ya 97 kwa mkwaju wa penalti.