COASTAL WAANZA KUIVUTIA KASI MBEYA CITY

BAADA ya kumaliza kazi mbele ya Dodoma Jiji kwa ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga hesabu zao kwa sasa ni mbele ya Mbeya City.

Mabao ya Coastal Union yenye maskani yake pale Tanga yalipachikwa na kijana Abdul Suleiman ambaye ameitwa pia kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars huku lile la Dodoma Jiji likifungwa na Anuary Jabir.

Kocha Mkuu wa Coastal Union Juma Mgunda amesema kuwa vijana wake wametimiza majukumu kwa umakini jambo lililowapa matokeo.

“Pongezi kubwa kwa vijana wangu kwa kuwa wamefanya kazi kubwa na nzuri kupata matokeo hilo ni jambo la msingi na tunakwenda kufanya maandalizi kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Mbeya City,”.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine ni Mei 24 ambapo Mbeya City wao mchezo wao uliopita wametoka kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya KMC.