AZAM FC YASEPA NA POINTI TATU MANUNGU

AZAM FC leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa mzunguko wa pili ambao umechezwa Uwanja wa Manungu, Morogoro.

Ushindi huo unaifanya Azam FC kusepa na pointi tatu Uwanja wa Manungu leo Mei 21 na kufikisha pointi 36 kibindoni.

Azam FC wakiwa wametoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Simba, Uwanja wa Azam Complex wameibuka na ushindi huo ugenini.

Mabao yote mawili yamepachikwa na nyota Ayoub Lyanga ambaye alitupia dk ya 20 na 54 hivyo kwenye kila kipindi nyota huyo alikuwa anatupia bao.

Kwa upande wa Mtibwa Sugar ni Said Ndemla ndiye ambaye alipachika bao pekee la kufutia machozi ilikuwa dk ya 80.