PABLO:HATUNA PRESHA NA YANGA

PABLO Franco,Kocha Mkuu wa Simba amesema wapinzani wao Yanga kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali haiwapi presha kwa kuwa wanaamini watafanya maandalizi mazuri.

Zimebaki siku 7 kabla ya watani hawa wa jadi hawajakutana kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mei 28.

Pablo amesema kuwa anawatambua wachezaji wake namna walivyo pamoja na wapinzani wao hivyo hawapati shida kuweza kuwakabili.

“Yanga tutakutana nao kwenye mchezo wa nusu fainali, wao walitangulia na sisi tumefuata hivyo huwezi kuzuia hilo kutokea kwa kuwa tutakutana nao hilo halitupi shida.

“Kila mchezo ni maandalizi na muda wa maandalizi wa mchezo wetu wa hatua ya nusu fainali tunajua namna ambavyo tutajipanga kuwakabili wapinzani wetu hao wajao,” alisema Pablo.