LALA SALAMA NDANI YA LIGI INAHITAJI UMAKINI

MWENDO unazidi kusonga kwa sasa kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa ni lala salama ya moto na yenye ushidani mkubwa.

Wakati wa kupanda kile ambacho ulikuwa unastahili ni sasa na ambaye ataweza kushinda atacheka na yule ambaye atashindwa tabasamu litayeyuka kwake.

Huu ni mzunguko ambao unakwenda kuamua nani anakuwa bingwa na nani anakwenda kushuka daraja kwa kuwa kule Championship tayari timu ambazo zimepanda zimejulikana.

Ihefu walikuwa wa pili kujihakikishia nafasi ya kupanda baada ya DTB kuweza kufanya hivyo na kuwa na tiketi ya kushiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.

Hapa kazi inamaanisha kwamba mwendo wao ndani ya Championship umekamilika kinachofuata ni changamoto mpya kwenye ligi.

Kushikana kwa sasa kwa wachezaji kwenye msako wa ushindi ni muhimu na kila mmoja anapswa kuendelea kuwa kwenye hesabu za kusaka ushindi nina amini hilo linawezekana kwa kila mmoja kucheza kwa umakini.

Hesabu kubwa za kusaka ushindi, umakini mkubwa uwanjani pamoja na ulinzi kwa kila mchezaji ni muhimu kuweza kutimiza majukumu kwa umuhimu zaidi.

Kwa sasa kuna wachezaji kandarasi zao zinameguka huku wengine wakiwa kwenye mazungumzo na timu nyingine ambazo zinahitaji saini zao.

Jambo kubwa kwa sasa kuweza kupata ushindi ni hesabu za kufanya kwa kuwa ushindi ni mbinu na kujituma ndani ya uwanja.

Ushindani ambao unaendelea kwa sasa acha uendelee kwa kuwa ilikuwa hivyo tangu mwanzo wa msimu hivyo kila timu mahali ilipo inaonesha kwamba inastahili.

Malengo ya kila timu kwa sasa yanasomeka kwenye zile mbao zao za malengo ambazo walikuwa nazo awali hivyo ni muhimu kuendelea kupambana bila kuchoka.

Wapo ambao walikuwa wanahitaji kubaki ndani ya tano bora na wapo ambao hesabu zao kubwa ni kubaki ndani ya ligi hivyo ni muda wa kukamilisha hesabu hizo sasa.

Ikiwa malengo ilikuwa ni kuwa ndani ya tano bora hata akiwa nafasi ya tano ama ya tatu hakuna ambacho amepoteza malengo yatakuwa yametimia.

Kushindwa kufikia malengo huwa inaumiza kwa sababu wengi wanadhani kwamba kazi ilikuwa ngumu hivyo jambo ambalo watafanya ni kuongeza nguvu katika kwa wakati ujao.

Matukio yale ya kuumizana kwenye mechi za ligi pamoja na Championship kwa wakati huu yasipewe nafasi kwani mchezaji akiumizwa sasa kazi yake inavurugwa kabisa na atakuwa na kazi ya kutibu alichoumia.

Wote wachezaji na benchi la ufundi ni muhimu kuweza kufanya kazi kwa kushirikiana ili kupata ushindi kwenye mechi ambazo zimebaki.

Wale ambao wanacheza kwa mkakati wa kumtoa mchezaji mchezoni kwa sasa ni muhimu kuacha badala yake iwe ni kucheza kwa kulindana ili wachezaji wasiumizane.

Mwisho wa msimu mchezaji akiumia huwa inakuwa jukumu lake kujitibu na wakati mwingine timu huvunja mikataba ya wachezaji hivyo afya ni jambo la msingi.