USHINDANI unazidi kuwa mkubwa kila iitwapo leo hivyo nafasi inapopatikana ni lazima kufanya kweli bila kuogopa.
Kila kitu kinawezekana na muda wa kufanya hivyo ni sasa baada ya kuwa kwenye kazi ngumu kutimiza kwenye mechi ambazo walianza awali kucheza na kupata ushindi.
Ni timu ya Taifa ya Wasichana U 17 ambayo inapeperusha bendera ya Tanzania kimataifa kwa kusaka tiketi ya Kufuzu Kombe la Dunia.
Ikumbukwe kwamba msafara wake Mei 19 uliweza kuanza safari kwa ajili ya kuelekea nchini Cameroon huko wana kazi ngumu ya kufanya.
Tunaamini kwamba safari yao haikuwa bure hasa ukizingatia ambacho wanahitaji ni ushindi kwenye mchezo wao ujao wa kimataifa.
Ni mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia ambao unatarajiwa kuchezwa Mei 22, 2022 kwenye mji wa Yaoundé.
Kila la kheri wapambanaji wetu na tunaamini kwamba mtapata matokeo mazuri kwenye mchezo huo muhimu kwa kuwa malengo ya kila timu ambayo inakwenda uwanjani ni kutafuta ushindi.
Ukweli ni kwamba mchezo hautakuwa mwepesi hasa ukizingatia kila timu inahitaji ushindi hivyo dk 90 zitakuwa ni za kazi kwelikweli.
Imani yetu na maombi ni kwenu mfanye vizuri ili mchezo wa marudio hapa Dar iwe kazi ya kumalizia kile ambacho mlianza.
Kila la kheri timu ya Taifa ya Tanzania kwenye majukumu yenu na tunaamini kwamba kwa maandalizi ambayo mlianza kufanya hapa Dar kazi itakuwa ni kufuata yale maelekezo ambayo mlipewa na benchi la ufundi.